Kamati ya Kudhibiti Uadilifu ya Chuo Kikuu cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (KKU – SUA) iliundwa rasmi mwaka 2018 kwa madhumuni ya kutimiza na kutekeleza Majukumu yafuatayo;
- Kuandaa na kutekeleza Mpango Kazi wa Mapambano Dhidi ya Rushwa wa taasisi husika, kuandaa taarifa za utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini za robo mwaka na mwaka na kuwasilisha kwa Kamati ya Uongozi ya Usimamizi
- Kupokea, kuchambua na kushughulikia malalamiko toka ndani na nje ya SUA yanayotokana na ukiukwaji wa maadili. Kamati pia itachukua hatua kwa muda unaofaa au muda usiozidi siku saba kwa malalamiko ya kawaida
- Kushiriki katika kutoa mafunzo kuhusu maadili, utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa kwa maafisa wa ngazi za kati, mameneja na watumishi wa kawaida
- Kuhakikisha kanuni za maadili na mienendo ya Utumishi wa Umma zinaeleweka kwa ufasaha miongoni mwa watumishi wa SUA
- Kuhakikisha mafunzo ya awali kuhusu maadili ya Utumishi wa Umma yanatolewa kwa watumishi na waajiriwa wapya SUA
- Kuishauri menejimenti ya SUA kusimamia na kutekeleza Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.