Wawakilishi wa KKU na Majukumu yao

Ili kuongeza ufanisi katika majukumu yake, KKU-SUA ina wawakilishi katika masuala ya Uadilifu kutoka katika Ndaki/ Kurugenzi/ Idara za SUA / Kampasi za SUA ambazo zipo mikoa mingine (e.g. Mazumbai, Olmotonyi, Katavi, Tunduru)/ na Kutoka Jumuiya ya Wanafunzi –

  1. Kwa upande wa Jumuiya ya Wanafunzi kunakuwa na wawakilishi wawili ambao wanapatikana kwa ushirikiano na Ofisi ya Mshauri wa Wanafunzi
  2. Muwakilishi mmoja anatakiwa awe mwanamke mwingine awe mwanaume.
  3. Wanapomaliza masomo yao, wawakilishi wengine wanachaguliwa

Wajibu wa Wawakilishi

  1. Kuwa kiungo kati ya KKU na Ndaki/Kurugenzi/Shule Kuu/ Idara, na Kampasi za SUA nje ya Mkoa wa Morogoro/ Jumuiya ya Wanafunzi katika masuala ya uadilifu
  2. Kuwasiliana na wafanyakazi/Jumuiya ya Wanafunzi kuhusu masuala ya uadilifu
  3. Kupokea taarifa na malalamiko kuhusu ukiukwaji wa maadili yakiwemo masuala ya rushwa kutoka kwa wafanyakazi/ Jumuiya ya Wanafunzi
  4. Kuwasilisha taarifa zinazohusu masuala ya uadilifu/ malalamiko kuhusu ukiukwaji wa maadili kwenye KKU
  5. Kubaini na kuishauri KKU katika masuala ya uadilifu
  6. Kufikisha taarifa (mrejesho) kwa Jumuiya ya Wanafunzi, kama zitakavyokuwa zinapatikana katika vikao vya KKU
  7. Kushiriki kwa dhati katika suala zima la mapambano dhidi ya rushwa na uadilifu na kujiepusha na majungu katika maeneo ya kazi/masomo
  8. Kuwasilisha taarifa zozote za malalamiko zinazohusu chuo kutoka vyanzo mbalimbali k.m. mitandao ya kijamii, vyombo vya habari, n.k. kwa KKU